Main Menu

Tuesday, October 29, 2013

PAMBANO LA SIMBA, AZAM LAINGIZA MIL 64/-

Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Azam lililochezwa jana (Oktoba 28 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 64,261,000.

Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 76 iliyomalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 walikuwa 10,728 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 9,802,525.42, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,793,490 wakati kila klabu ilipata sh. 14,946,170.45.

Wamiliki wa uwanja walipata sh. 7,599,747.49, gharama za mchezo sh. 4,599,848.61, Bodi ya Ligi sh. 4,599,848.61, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,279,924.31, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,773,274.46.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

0 comments:

Post a Comment