Klabu ya Toto African ya Mwanza inatarajiwa kufanya
uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi katika kamati yake ya utendaji ifikapo
tarehe 11 Oktoba 2015. Katika barua yake kwa Katibu Mkuu wa Toto African,
Katibu Mkuu wa TFF ameuagiza uongozi wa Toto African kuwasiliana na Kamati yao
ya Uchaguzi ili tangazo la uchaguzi litolewe si chini ya siku sitini (60) kabla
ya tarehe ya kufanyika uchaguzi.
Kwa muda mrefu kumekuwa na mvutano katika klabu ya Toto
na suala kubwa likiwa ni kuhusu ujazaji wa nafasi zilizo wazi. Awali TFF
ilipokea maombi ya wanachama na wadau wa Toto African wakitaka ufanyike
uchaguzi ili kumaliza mvutano ndani ya klabu.
TFF ilishauri uchaguzi huo kusubiri klabu kukamilisha
mchakato wa usajili.
Vilevile TFF imewataka wadau wote wa klabu hiyo kongwe ya
mjini Mwanza kuheshimu uongozi uliopo madarakani kwani ndio unaotambulika na
ndio utaendelea kuiongoza Toto African katika kipindi cha kuelekea uchaguzi
uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment