Timu
ya Red Arrows inayoshiriki Ligi Kuu nchini Zambia, kesho siku ya alhamis
itashuka uwanja wa Karume kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Kiluvya
United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania bara.
Mchezo
huo wa kirafiki ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo kutoka nchini Zambia
ambayo imeweka kambi jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya
wa Ligi Kuu nchini Zambia.
Mara
baada ya mchezo huo, Kikosi cha Red Arrows kitaendelea na mazoezi kwenye uwanja
wa Karume na Ufukwe wa Mbalamwezi kulingana na ratiba ya kocha wa timu hiyo.
Red
Arrows watacheza mchezo wao wa pili na mwisho wa kirafiki siku ya jumapili
dhidi ya timu ya Ruvu Shooting inayoshiriki Ligi Kuu (VPL), mchezo ambao
utachezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es salaam kabla ya kumaliza ziara
yao siku ya jumanne na kurejea nchini Zambia.
0 comments:
Post a Comment