Watu wasiopungua 14 wamefariki dunia katika mji wa Port Said nchini Misri baada ya kuzuka ghasia kubwa.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, ghasia hizo zimeibuka baada ya Mahakama ya Jinai ya Misri kutoa hukumu ya kifo kwa watu 21 waliopatikana na hatia ya kushiriki katika ghasia za Februari mwaka jana zilizotokea kwenye uwanja wa mpira wa miguu baada ya mechi iliyozikutanisha klabu mbili za al Ahly na al Masry katika mji wa Port Said.
Watu wasiopungua 72 waliuawa katika ghasia hizo.
Taarifa ya mahakama hiyo imebainisha kwamba, hukumu ya watu wengine 52 waliobakia inatarajiwa kutolewa Machi 9 mwaka huu.
Taarifa zaidi zinasema, ghasia kubwa zilizuka leo baina ya waandamanaji na maafisa wa polisi.
Rais wa misri muhammad mursi
Katika ujumbe wake kwa wananchi wa Misri aliotoa katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter Rais Mursi amewataka wananchi wa nchi hiyo kudumisha amani na utulivu.
0 comments:
Post a Comment