ngasa akipiga pushap baada ya kufunga bao la tatu
SIMBA SC leo imeanza vyema mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa African Lyon ya
Dar es Salaam mabao 3-1 katika mchezo wa ufunguzi wa duru ya pili.
Hadi mapumziko Simba SC tayari
walikuwa mbele kwa mabao 3-0, yaliyotiwa kimiani na Mrisho Khalfan Ngassa
mawili dakika za 19 na 39 na Ramadhan Suleiman Chombo ‘Redondo’ dakika ya tatu
ya mchezo huo.
Redondo aliifungia Simba SC bao la
kwanza dakika ya tatu, akiunganisha krosi nzuri ya Ngassa kutoka wingi ya
kushoto na kufumua shuti akiwa katikati ya msitu wa mabeki wa Lyon.
MATOKEO
YA MECHI NYINGINE
Mtibwa Sugar 0-1 Polisi Morogoro
Coastal Union 3-1 Mgambo JKT
Ruvu Shooting 1-0 JKT RUVU
Azam FC 3-1 Kagera Sugar
JKT Oljoro 3-1 Toto Africans
KESHO; Januari 27, 2013
Yanga SC Vs TZ Prisons
0 comments:
Post a Comment