Kikosi kipya cha mapambano cha Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza
kimezishambulia ngome za waasi wa harakati ya Machi 23 huko mashariki
mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu kuundwa kikosi hicho mapema
mwaka huu kwa lengo la kupambana na makundi ya waasi wenye silaha.
Maafisa wa kijeshi wa Umoja wa Mataifa na wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo wamesema kuwa kikosi hicho cha uingiliaji kati ambacho kina
mamlaka makubwa ikilinganishwa na vikosi vingine vya kulinda amani vya
Umoja wa Mataifa, kinalisaidia jeshi la Kongo katika mapambano yake
dhidi ya waasi wa M23.
Kanali Olivier Hamuli msemaji wa jeshi la Kongo
amesema kuwa kikosi cha mapambano cha Umoja wa Mataifa kiko upande wao
na kwamba kinawapatia silaha vikosi vya Kongo.
Raia wa Kongo wasiopungua
wanne waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya nyumba kadhaa
katika maeneo ya raia huko Goma kuangukiwa na makombora juzi Alkhamisi.
na radio tehran
Friday, August 23, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment