Main Menu

Friday, August 23, 2013

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 MKOANI TABORA KATIKA UWANJA WA AL-HASAN MWINYI.......NOUMA SAAANA


 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia mbele ya wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi  kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Abdul Kiba,msanii wa muziki wa bongofleva akiimba mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humo.
 Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humo.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah pichani kati akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani  kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 .
 Anaitwa Amin,mmoja wa wasanii mahiri akiwaimbisha mashabiki wake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani tabora 
 Ni shwangwe tu
Wakali wa kudansi kutoka THT,wakijulikana kwa jina la Makomanda wakionesha umahiri wao wa kucheza jukwaani  kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
 Wanamuita Mzee wa Masauti,Christian Bella akiwaimbisha mashabiki wake wa muziki wa dansi.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 wakiwa wamewasha tochi za simu zao wakiashiria kushoo love ya pamoja
Msanii wa muziki wa bongofleva,Rachael akicheza jukwaani na mmoja wa madensa wake,huku mashabiki wake wakipiga mayowe ya shangwa kuonesha kukunwa vilivyo na msanii huyo.
 Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.


0 comments:

Post a Comment