Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Juliana Yassoda (Katikati) akiongea na
Wanahabari kuhusu makocha wa Timu ya Barcelona kutoka
nchini Hispania ambao wako nchini kwa ajili ya mafunzo ya makocha
yatakayofanyika kwa muda wa siku mbili, wa kwanza kulia ni Balozi wa
Spain nchini Mh. Luis Manuel Ceuesta Civis.
Kocha
Isaac Oriol Guerrero Hernandes (katikati) kutoka timu ya Barcelona ya
nchini Hispania (katikati) akitoa maelezo kwa wanahabari (hawapo
pichani) kuhusu mafunzo ya siku mbili watakayotoa kwa makocha 30
wakizalendo, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana
Bi. Juliana Yassoda na wa kwanza kushoto ni Kocha Daniel Bigas Alsina.
Balozi
wa Hispania nchini Tanzania Mh. Luis Manuel Ceuesta Civis (Kulia)
akiongea na Makocha kutoka Timu ya Barcelona ya nchini Hispania katika
mkutano wa Wanahabari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana (leo),
makocha hao wapo nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo ya siku mbili kwa
makocha wazalendo, wa kwanza kushoto ni Kocha Daniel Bigas Alsina na
katikati ni Kocha Isaac Oriol Guerrero Hernandes.
Makocha
wa Kizalendo 30 ambao wanatarajiwa kupewa mafunzo ya siku mbili kutoka
kwa makocha wa Barcelona wakiwa katika picha ya pamoja..




0 comments:
Post a Comment