Rais wa serikali ya mpito ya Madagascar amekubali kuondolewa jina lake
miongoni mwa majina ya viongozi wasiostahiki kuwa wagombea wa kiti cha
urais nchini humo.
Rais Andry Rajoelina wa serikali ya mpito ya
Madagascar jana alikubali rasmi kuondolewa jina lake miongoni mwa
wagombea wanaofaa kushiriki katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo.
Amesisitiza kuwa atakabidhi madaraka kwa njia ya kidemokrasia kwa rais
atakayechaguliwa nchini humo baada ya kufanyika uchaguzi.
Hii ni katika
hali ambayo Lalao Ravalomanana mke wa Rais wa zamani wa Madagascar
amepinga uamuzi wa mahakama maalumu ya uchaguzi ya kuliondowa jina lake
katika orodha ya wagombea wa kiti cha urais .
NA radio tehran
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment