Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha
mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga, Pan Africans na Taifa Stars,
Athuman Kilambo kilichotokea jana (Machi 10 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam.
Msiba
huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti
Kilambo akiwa mchezaji, na baadaye kocha alitoa mchango mkubwa kwa timu
mbalimbali alizochezea na kufundisha zikiwemo Pan Africans na Cargo,
hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF
inatoa pole kwa familia ya marehemu Kilambo, Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya Pan Africans na kuwataka kuwa
na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Maziko
yanatarajiwa kufanyika leo (Machi 11 mwaka huu) katika makaburi ya
Kisutu mkoani Dar es Salaam ambapo TFF imetoa ubani wa sh. 100,000.
Mungu aiweke roho ya marehemu Kilambo mahali pema peponi. Amina
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment