Ubinafsi wa wa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi usiku wa jana umemnyima hat trick mshambuliaji Luis Suares baada ya kung'ang'ania kupiga penalt ambayo hata hivyo alikosa.
Suarez ambaye jana aliweka kambani mabao mawili alikua na nafasi ya kuondoka na mpira wakati ilipopatikana penalt katika dakika za mwisho za mchezo huo penalt iliyopigwa na Messi.
Kitendo cha Messi kupiga penalt hiyo kimetafsiriwa kama ubinafsi ambao mara nyingi Messi amekua akihusishwa nao katika kikosi cha Barca.
Katika mchezo wa jana uliopigwa katika dimba la Etihad Barca waliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa kwa moja mabao yaliyofungwa na Luis Suares huku bao la kufutia machozi la City likifungwa na Kun Aguero.
Luis Suarez akifunga goli la kwanza mbele ya beki wa Manchester City captain Vincent Kompany
Suarez akishangilia goli lake la kwanza katika mchezo wa klabu bingwa barani ulaya hatua ya 16 katika dimba la etihad jijini manchester.
Suarez, kwa mara nyingine akishangilia goli la pili la barcelona
Kompany, Fernando na James Milner
wakiwa na nyuso za masikitiko baada ya kipigo cha mabao mawili kwa moja.
Sergio Aguero akiifungia city bao la kufutia machozi huku akishuhudiwa na wilfred boni aliyeingia kuchukua nafasi ya from David Silva
Gael Clichy akioneshwa kadi nyekundu katika mchezo huo
penalt ya Lionel Messi ikiokolewa na kipa wa city Joe Hart.
messi baada ya kukosa penalt na hata alipopiga kichwa kilikwenda nje.
0 comments:
Post a Comment