Kamati ya Utendaji
ya Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF iliyokutana jumapili Februari 22 mwaka
huu, imefanya mabadiliko ya mahali utakaofanyika Mkutano Mkuu wa mwaka kutoka
Mkoa wa Singida na kuhamishia mkoa wa Morogoro.
Hatua hiyo
imefikiwa na Kamati ya Utendaji kutokana na sababu za kutokukamilika kwa
miundombinu ya mkutano mkuu na kuwepo kwa shughuli nyingine za kijamii mkoani humo.
Kamati ya Utendaji
inamshukuru Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Singida (SIREFA), na
uongozi mzima kwa kujitolea kuandaa mkutano huo na huko nyuma waliweza kuandaa
mkutano wa makatibu wa vyama vya soka vya mikoa.
TFF itaandaa vikao
na matukio mengine mkoani Singida itakapotokea hapo baadae, tarehe ya mkutano
mkuu itaendelea kubakia ile ile ya Machi 14, 15 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment