Mwenyekiti wa
baraza la michezo la Taifa, Dioniz Malinzi amelitaka shirikisho la soka nchini
kuwawajibisha waamuzi wanaoharibu mpira wa miguu nchini.
Malinzi ameyasema
hayo wakati akifunga mafunzo ya waamuzi vijana 35 kutoka mikoa mbalimbali
nchini yaliyokua yanafanyika katika uwanja wa Karume Dar es salaam.
Amesema haiwezekani
viongozi wa TFF wanakuwepo uwanja wa taifa na waamuzi wanaruhusu magoli yasiyo
halali nab ado katika mchezo ujao unawaona tena wapo katikati ya uwanja kisa
unasubiri ripoti ya msimamizi.
“Tuna matatizo
mengi katika michezo lakini tatizo kubwa ni waamuzi ambao wanatuharibia mpira
wetu kwa sababu ya tamaa na ubinafsi
badala ya kuwafikiria watanzania wanafikiria matumbo yao”amesema malinzi.
Malinzi amefika
mbali zaidi hadi kuhoji au viongozi hao nao wanapewa mgao wa rushwa wanaopewa waamuzi
kwa sababu haiwezekani ukashuhudia upuuzi wa waamuzi na bado ukakaa kimya bila kuchukua hatua yoyote.
“Ni kazi
bure timu kutumia mamilion ya fedha kujiandaa alafu mwisho wa siku anakuja mtu
mmoja kusimama katikati ya uwanja na kuharibu ladha ya mchezo kwa kutoa maamuzi
yasiopendeza”amesema.
Mwenyekiti huyo
amesema itakua ni kazi bure kuwaandaa vijana wadogo kuwa waamuzi alafu
wanawaona wakubwa wao wanaharibu mpira na wahachukuliwi hatua yoyote.
Amesema mpira
ni mali ya TFF na sio bodi ya ligi wala kamati ya waamuzi, hivyo chochote
kitakacho haribika wakuulizwa ni TFF, hivyo ameitaka TFF iwe strong kusimamia
mpira na kuondoa upuuzi wote unaoendelea.
“Haiwezekani
televishen zimeonesha, viongozi wa TFF walikua uwanjani wameona madudu ya
waamuzi alafu kwenye ripoti hakuna maelezo yanayoeleka na bado mnaakaa kimya
haiwezekani”amesema.
Mwisho Dioniz
Malinzi amelitaka shirikisho hilo kuboresha maslahi ya waamuzi labda inaweza
kupunguza ushawishi wa kupokea rushwa kwani haiwezekani mchezo uingize sh. million
70 mwamuzi anapewa laki mbili…..tena anasafirishwa kwa basi kutoka Musoma kuja
dar.
Kamaliza kwa
kuwahusia vijana hao kuwa mbali na rushwa kwa sababu rushwa ni adui wa haki.
0 comments:
Post a Comment