Katika kuongeza
motisha kwa waamuzi na kuwashawishi kuchezesha kwa haki mwenyekiti wa baraza la
michezo la taifa ameahidi sh. Million 5 kwa mwamuzi bora.
Akifunga kozi
ya waamuzi vijana 35 kutoka mikoa mbalimbali nchini Dioniz Malinzi amesema yupo
tayari kutoa zawadi ya sh. Million 5 kwa
muamuzi wa kati na sh. Million 2 kwa mshika kibendera bora.
Lakini malinzi
ametoa masharti kwa TFF kutoa mchanganuo wa namna walivyompata mwamuzi bora na
sababu za kuwa bora.
Amesema labda
zawadi hiyo inaweza kuchangia waamuzi nchini kutenda haki na kuzisaidia timu
zetu kushindana kikamilifu katika michuano ya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment