Main Menu

Friday, May 3, 2013

LEO NI SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI


Tanzania leo imeungana na mataifa mengine duniani katika kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, wanadiplomasia na wanasiasa wanatarajia kukutana.

Maadhimisho hayo ambayo kitaifa yatafanyikia jijini Dar es alaamu ambapo mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Richard Sezibera.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa maandalizi ya maadhimisho hayo amabae ni  Mkurugenzi wa Taasisi za Vyombo vya Habari vya Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania Tumaini Mwailenge amesema maadhimisho hayo yatahusisha washiriki zaidi ya 200 kutoka nchi za Afrika Mashariki.

Amesema watakaoshiriki maadhimisho hayo ni wamiliki wa vyombo vya habari, wahariri na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari huku kaulimbiu ya maadhimisho hayo  inasema  USALAMA NA MAZINGIRA BORA YA KAZI KWA WAANDISHI.
 
Mwailenge ameongeza kuwa mbali na masuala ya usalama wa waandishi, pia wanazikumbusha Serikali  juu ya masuala ya uwepo wa mazingira bora ya waandishi kufanyia kazi, changamoto za binadamu katika nchi za Afrika Mashariki lakini pia wamekusudia kuanzisha mfuko Maalumu wa David Mwangosi, lengo ikiwa ni kumuenzi.

Mkoa wa iringa  unaadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari katika  ukumbi wa halmashauri kwa mijadala mbalimbali, harambee ya kutunisha Ipc Vikoba, pamoja na uzinduzi wa ofisi, ambapo mijadala hiyo itatanguliwa shughuli za kufanya usafi katika baadhi ya maeneo ya mji huo
.

0 comments:

Post a Comment