meneja wa tbl na mwenyekiti wa ccm mkoa wa iringa jesca msambatavangu
meneja wa tbl mkoa wa iringa josephat changwe akimkabidhi vifaa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kwa ajili ya kugawa kwa vyuo shiriki
kaptan wa chuo cha ruco akipokea vifaa kutoka kwa diwani wa kata ya kitanzia na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa iringa jesca msambatavangu.
kaptani wa chuo cha cdti akipokea vifaa
kaptan wa timu ya chuo cha ruco na timu ya taifa kushoto akishukuru kwa vifaa
Mashindano
ya Safari Lager Higher Learning Pool Competition kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya
mkoa wa Iringa yanatarajiwa kufanyika tarehe 4 mwezi huu siku ya jumamosi.
Akizungumza
na waandishi wa habari mwenyekiti wa chama cha Pool mkoa wa Iringa Salum Kisaku
amesema mashindano hayo yatashirikisha vyuo vinne mkoani humo ambavyo ni
Tumaini, Ruco, Mkwawa na chuo cha maendeleo ya jamii ( CDTI) ambayo
yanatarajiwa kufanyika club Twisters mkoani humo.
Amesema
mshindi wa mashindano hayo mbali ya kupata zawadi atauwakilisha mkoa katika
katika mashindano ya kitaifa yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam hapo
baadae.
Kwa upande
wao wadhamini wa mchezo huo TBL kupitia meneja wake mkoa wa Iringa Josephat
Change ameelezea jitihada za kampuni hiyo kuuinua mchezo huo ambao umeendelea kuwa maarufu hapa nchini.
amesema jitihada za tbl ni kuufanya mchezo huo kuchezwa na kila mtu kuanzia umri mdogo tofauti na ilivyo sasa ambapo watu wengi wanaamini mchezo huo ni wawa levi na unachezwa kwenye bar.
mashindano hayo ambayo yatafanyika siku ya jumamosi ya tarehe 4 may club twisters mkoani iringa, mshindi wa kwanza kwa chuo atapata sh laki tano, mshindi wa pili laki nne, mshindi wa tatu laki tatu.
kwa upande wa mchezaji mmoja moja wanaume, mshindi wa kwanza laki moja na nusu na mshindi wa pili laki moja.
kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja wanawake, mshindi wa kwanza laki moja na mshindi wa pili elfu hamsini.
0 comments:
Post a Comment