Friday, April 17, 2015
CHELSEA VINARA WA UKOROFI LIGI KUU YA ENGLAND
Kuelekea katika mchezo wa Ligi kuu ya soka nchini England kati ya Chelsea na Manchester United hapo kesho, klabu ya Chelsea inatajwa kuwa ndiyo timu inayoongoza katika Ligi kuu ya England kwa kutowaheshimu waamuzi wa ligi hiyo.
Takwimu hizo zimetolewa na jarida la kila siku la nchini England linalofahamika kama Daily Telegraph, Kwa mujibu wa jarida hilo klabu ya Chelsea inaongoza huku nafasi ya pili ikishikwa na klabu ya Sunderland.
Wakati wachezaji wa Chelsea wakiwa wanaongoza kwa kutowaheshimu waamuzi kama kuwazonga na kuwatolea maneno makali, benchi la ufundi la Chelsea linashika nafasi ya pili kwa kutotii sheria za ndani ya uwanja ikiwa ni pamoja na kuheshimu mstari uliowekwa kama mpaka kati ya benchi la ufundi na benchi la ufundi lakini pia kutoingia ndani ya uwanja.
Lakini pia kwa mujibu wa jarida hilo, klabu ya Liverpool ndiyo klabu yenye nidhamu ambayo ni nadra kuona wachezaji wakiwazonga waamuzi na kuwatolea maneno makali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment