Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea kesho siku ya ijumaa kwa mchezo mmoja,
wenyeji timu ya Stand United watawakaribisha maafande wa JKT Ruvu katika uwanja
wa Kambarage mjini Shinyanga.
Ligi hiyo ya
Vodacom itaendelea kutimua vumbi siku ya jumamosi kwa michezo mitatu, mjini Morogoro wenyeji
Polisi Morogoro watawakaribisha Ndanda FC kwenye uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro.
Jijini Mbeya
wenyeji timu ya Mbeya City watawakaribisha timu ya Simba SC kwenye uwanja wa
Sokoine , huku Azam FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar kwenye
uwanja wa Chamanzi Complex.
Jumapili Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania itaendelea kwa
maafande wa timu ya Ruvu Shooting
kuwakaribisha maafande wenzao wa Mgambo Shooting katika uwanja wa
Mabatini - Mlandizi, huku jijini Mbeya wenyeji timu ya Prisons FC wakiwakaribisha
wakata miwa wa Mtibwa Sugar.
0 comments:
Post a Comment