Haya twende! Timu ya Help for Underserved Communities (HUC) ikishirikiana na Lifetime Wells for Ghana Inc., wakichimba moja ya visima 59 Wilaya ya Kilombero, Morogoro, huku wakiangaliwa kwa shauku na watoto hivi karibuni. HUC ni asasi isiyokuwa ya kiserikali yenye makao yake Marekani, inayochimba visima kwa kushirikiana na jamii kusaidia upatikanaji wa maji ya kunywa safi na salama mashuleni, vijijini na jamii kwa ujumla.
Wachimba visima toka Help for Underserved Communities (HUC) na Lifetime Wells for Ghana Inc., kama walivyokutwa na kamera yetu Wilaya ya Kilombero, Morogoro, wakati wa uchimbaji visima vya msaada uliotolewa na taasisi hizo hivi karibuni.
Wakazi wa Kilombero wakiangalia kisima kilichochimbwa na Help for Underserved Communities (HUC) kwa ushirikiano na Lifetime Wells for Ghana Inc., Wilaya ya Kilombero, Morogoro, hivi karibuni.
Uchimbaji ukiendelea.
Dalili ya matumaini, maji bwelele.
(Picha zote na Nathan Mpangala wa HUC)
0 comments:
Post a Comment