Main Menu

Sunday, May 10, 2015

TFF YAKUBALI UENYEJI KAGAME CUP



Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, leo hii imekubali kuwa wenyeji wa  michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ngazi ya Vilabu maarufu kama CECAFA Kagame Cup.

Tff imekubali ombi hilo baada ya cecafa kutuma maombi kwa Tanzania kuwa mwenyeji mwezi uliopita.

CECAFA ambao ndio wamiliki wa mashindano hayo watatoa mialiko kwa vilabu vyenye sifa ya kushiriki na wakipokea uthibitisho wa ushiriki wao watatoa orodha ya vilabu shiriki na ratiba ya michuano hiyo.

Ikumbukwe tu Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika nchini kuanzia tarehe 11 Julai mpaka 02 Agosti 2015.

0 comments:

Post a Comment