Main Menu

Sunday, May 10, 2015

TIMU YA MBEYA CITY YAJIPONGEZA KWA KUMALIZA KATIKA NAFASI YA 4



 
Baada ya kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa mwaka 2014/2015 iliyomalizaka jana, timu ya Mbeya City imetoa tuzo kwa wachezaji wake.

Nafasi walioipata Mbeya City msimu huu ni nafasi moja chini ya walioipata mwaka jana ambapo ndio ilikua msimu wao wa kwanza wa ligi kuu.

Tuzo hizo zimetolewa kwa wachezaji, viongozi na mashabiki ambao kwa pamoja wameshirikiana kuifanya timu hiyo ifike hapo ilipo baada ya kukabiliwa na tishio la kushuka daraja ikiwa imesalia michezo mitano.

Kocha mkuu wa kikosi hicho Juma Mwambusi alipewa tuzo ya kocha mwenye mafanikio na mstahimilivu kwa misimu miwili na kuiweka timu katika nafasi nzuri mfululizo.
 
Wachezaji Paul Nonga, Themi Felix na Deus Kaseke walipata tuzo za heshima kwa mchango wao kwenye timu kwa misimu miwili.

Wachezaji Rafael Alpha na Kenny Ally walipewa tuzo ya wachezaji chipukizi waliofanikiwa katika kikosi hicho.
Golikipa aliyekuja kuziba nafasi ya David Buruani,  Hamilton Telisibula amepewa tuzo ya kipa bora.

Mkongwe Juma Nyosso, Hassan Mwasapili na Peter Mwalihanzi wao wamepewa tuzo ya uchezaji bora hususani mzunguko wa pili.
 
Lakini wachezaji wengine 18 wamepewa zawadi mbalimbali sambamba na fedha taslim.

Hata hivyo timu hiyo kupitia kwa afisa habari wake Dismas Ten imeipongeza timu ya yanga kwa kuwa mabingwa wa ligi hiyo na kuwataka wajipange vilivyo kwa michuano ya kimataifa mwakani.

0 comments:

Post a Comment