Baada ya mahojiano kati ya mrufani
Dr Damas Ndumbaro na Wakili wa TFF Nd Emmanuel Muga, pamoja na
Wajumbe wa Kamati ya rufaa ya nidhamu kuwahoji wote, Mrufani na Wakili wa TFF,
Kamati ya rufaa ya nidhamu ilichukua uamuzi ufuatao:-
1.
Hoja ya kwanza cha rufaa, kwamba
kamati ya nidhamu haikuwa na nguvu za kisheria kusikiliza shauri lake, Kamati
ya rufaa ya nidhamu baada kusikiliza hoja za pande zote mbili, kwa uamuzi wa
Wajumbe wote kwa maana ya kuwa zote nne za Wajjumbe wa kamati ya rufaa ya
nidhamu, ilitupilia mbali hoja hiyo na kuona kwamba kamati ilikuwa na mamlaka
ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa mkata rufaa ni afisa wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania TFF kwa mujibu wa Katiba ya TFF ya 2013. Uamuzi katika hoja
hii uliamuliwa kwa kura 3 dhidi ya moja.
2.
Hoja ya pili inayosema kwamba kamati
ilikosea kisheria kwa kutompa muda wa kuleta utetezi wake wala vielelezo
vyovyote vile kwenye shauri lake.
Kamati ya rufaa ya Nidhamu kwenye
Shauri hili, baada ya kufanya maamuzi kwa kupiga kura, kura za Wajumbe watatu
zilitupiliwa mbali hoja yake na kura moja kati ya kura nne ilikubaliana na hoja
yake kwa uamuzi huo, kamati ya rufani ya nidhamu ilitupilia mbali hoja hiyo kwa
uamuzi wa wingi wa kura kwa maana ya kuwa tatu dhidi ya kura moja.
Sababu za kutupilia mbali hoja hizo
ni kwamba mrufani alipata wito wa kwenda kwenye shauri, na akawakilishwa na
wakili wake ( Nestory Peter Wandiba ) kwenye Shauri hilo. Shauri
liliposikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 10/10.2014 shauri lilipangwa
kusikilizwa tarehe 11/10/2014 Lakini siku hiyo ya pili si wakili wala Dr
Ndumbaro alifika kwenye shauri hilo kwa maana hiyo basi shauri lililazimika
kusilikizwa upande mmoja kwa mujibu wa kanuni za nidhamu za TFF ibara ya 94
(3).
3. Hoja ya tatu linalosema kwamba kamati ilikosea kusiliza
shauri upande mmoja bila ya mtuhumiwa kuwepo, ni kukiuka haki yake ya msingi
ya kusikilizwa.
Kamati baada ya kusikiliza utetezi
kutoka pande zote mbili kamati ilifanya uamuzi kwa kupiga kura, na kura tatu
(wajumbe watatu) walitupilia mbali hoja hiyo, dhidi ya kura moja (mjumbe mmoja)
aliyeikubali hoja hiyo. Sababu za kutupilia mbali hoja hiyo ni kutokana na
ukweli kwamba mrufani alipata wito wa kuhudhuria shauri hili na akamtuma wakili
wake, lakini mrufani alishindwa kuonyesha vielelezo vya kuonyesha kwamba
angesafiri kwenda nje ya nchi ili kamati ya nidhamu iweze kuahirisha shauri
mpaka wakati ambao angekuwa amerejea lakini hakufanya hivyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa Ibara
144(2) (3) za kanuni ya nidhamu za TFF, mrufani angeweza pia kuomba
kamati ya nidhamu ibatilishe uamuzi iliyoutoa dhidi yake ili aweze kusikilizwa
utetezi wake pia hakufanya hivyo na aliamua kukata rufaa.
4. Hoja ya nne inayosema kwamba kamati ilikosea kisheria
katika uchambuzi wa ushahidi wa mlalamikaji na hatimaye kutoa uamuzi uliomtia
hatiani.
Kamati ya rufani ya nidhamu
ilisikiliza kwa umakini hoja za pande zote mbili na kujiridhisha kwamba mrufani
alifanya makosa kwa kutoa taarifa isiyosahihi na kupotosha maamuzi ya TFF
kinyume na kanuni ya 41 (6) ya kanuni za ligi kuu ya Tanzania toleo la 2014 (4)
na pia kushawishi, kupotosha au kuzuia maamuzi/utekelezaji wa maamuzi ya TFF
kinyume na kanuni ya 41(16) ya kanuni za ligi kuu za Tanzania ya (2014).
Wakati wa kufanya maamuzi, wajumbe
watatu(3) kwa maana ya kura tatu zilitupilia mbali hoja hiyo, na kura moja, kwa
maana ya mjumbe mmoja alikubaliana na hoja hiyo. Kwa maana hiyo, kamati ya
rufaa ya nidhamu ya TFF imetupilia mbali hoja hiyo.
Kwa uamuzi huu kamati inadhibitisha
uamuzi wa kamati ya nidhamu iliyosomwa tarehe 13/10/2014, uamuzi huu umefikiwa
baada ya wajumbe kupiga kura na uamuzi kupitishwa kwa wingi wa kura za wajumbe
watatu, dhidi ya mjumbe mmoja wa kamati hii kwa hoja ya 2,3 na 4 na wajumbe
wote 4 walikubaliana kutupiliwa mbali hoja ya kwanza.
Kwa hiyo Dr Damas Ndumbaro
ataendelea kutumikia adhabu yake kwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya Mpira
wa Miguu (Soka) kwa kipindi cha miaka saba.
Hata hivyo mrufani Dr Damas Ndumbaro
anayohaki ndani ya siku 10 kuanzia leo tarehe 10/05/2015 ya kuomba marejeo ya
uamuzi huu mbele ya kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF chini ya Ibara 142 ya
kanuni za nidhamu za TFF ya mwaka.
Kila upande utabeba gharama zake Hukumu
inasomwa leo tarehe 10/05/2015/
Revocatus L. K. Kuuli.
MAKAMU MWENYEKITI.
0 comments:
Post a Comment