Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
kesho jumatano inatarajiwa kusafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya
kushiriki michuano ya kombe la COSAFA.
Michuano ya COSAFA inatarajiwa kuanza
kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015 katika viwanja vya Olympia Park na
Moruleng jimbo la North West Province nchini Afrika Kusini ikishirikisha
nchi za Kusini mwa Afrika huku Tanzania na Ghana zikiwa ni nchi waalikwa.
Taifa Stars itaondoka jijini Dar es salaam
kesho majira ya saa 1 jioni, kwa usafiri wa shirika la ndege la Fasjet na
kufika jijini Johanesburg saa 5 usiku.
Mara baada ya kupimwa afya jana na
madaktari wachezaji Aishi Manula, Isihaka Hassan, Haroun Chanongo, Kelvin
Friday na nahodha Nadir Haroub wamekutwa na majeruhi ambayo yamepelekea
kutokuwepo katika kikosi kitakachosafiri kesho, watabakia nchini wakiendelea
kufanya mazoezi chini ya ungalizi mpaka timu itakaporejea kutoka Afrika Kusini
na kuungana kwa ajili ya maandalizi ya AFCON, huku Amri kiemba akipewa ruhusa
kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.
Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ephaphra Swai ukijumuisha wachezaji 20 na benchi
la ufundi, timu inatarajiwa kufikia katika hoteli ya Sun City iliyopo pembeni
kidogo ya jiji la Rusterburg.
0 comments:
Post a Comment