Main Menu

Friday, August 23, 2013

MDAU WENU ZIARANI MKOANI KILIMANJARO, MANISPAA YA MOSHI MJINI KATIKA MAPUMZIKO YA LIKIZO.

Mmoja kati ya mmiliki wa mtandao huu yahaya mohamedy akiwa eneo la YMCA mjini Moshi kwenye mzunguko ambao unazikutanisha barabara itokayo Dar es salaam, Kcmc, katikati ya mji na Arusha ambapo kuna sanamu ya askari jeshi ambayo imekua ikitambulika kama utambulisho wa mji wa Moshi kwa muda mrefu.
 

 Muonekano wa eneo hili unadhiirisha hali halisi ya mji wa Moshi kushika nafasi ya kwanza kwa usafi kati ya halmashauri zote nchini lakini pia umekua ukifanya vizuri pia kati ya miji barani Afrika, endelea kufuatilia mtandao huu kupata matukio mengi yakuvutia kutoka sehemu mbalimbali hususani kipindi hiki cha mapumziko.

Mnara huu umekuwa na story ya kuvutia na hata kuchekesha kwa ndugu zetu Wachaga waishio maeneo ya Kishumundu ambapo inasemekana kuwa miaka ya nyuma wakati wakileta ndizi kuuza Moshi mjini walikua wakifika kwenye mnara huu walikua wanatupa ndizi zao na kuanza kukimbia kwa kuogopa sanamu hilo, huku wengine wakipiga magoti kumuomba msamaha mjeshi sanamu huyo..............hahaha.

0 comments:

Post a Comment