Rais wa klabu hiyo Evans Aveva amesema kadi hizo zina
faida kubwa kwa wanachama wake pindi watakapopata matatizo.
Eveva amesema kadi hiyo mbali ya kumpa bima mwanachama
itakua ikiwachangia wanachama wake fedha kiasi cha shilingi 250,000 pindi
atakapofiwa na mke/mme, mtoto au yeye mwenyewe.
Kwa upande wake mkurugenzi wa EAG group Iman Kajura ambao
wana jukumu la kuitafutia wadhamini timu hiyo amesema kadi za watoto zimelenga
kuwaweka watoto karibu na timu hiyo tofauti na ilivyo sasa watoto wengi
wanazijua zaidi timu za ulaya.
Mpango huu wa kadi za uanachama ni tofauti na ule wa kadi
za mashabiki walizoingia mkataba na Bank ya Posta.




0 comments:
Post a Comment