Mratibu wa mashindano ya Iringa super cup na
mwenyekiti wa klabu ya Lipuli ya Iringa Abou Majeki akipokea msaada ya
mipira kutoka kwa mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa Emma Kuhanga ambao ni
kati ya wadhamini wa mashindano hayo yanayofanyika mjini Iringa.
Katibu mkuu wa chama cha soka mkoa wa Iringa
ELiud Peter Mvela akipokea cheki ya milioni 14 na laki 5 kutoka kwa rais
wa Lipuli madam Jesca Msavatavangu rasmi kuichukua Mkwawa stars
football club zamani ikijulikana polisi Iringa.
Taasisi ya kuzuia na
kupambana na Rushwa mkoani Iringa leo imekabidhi mipira miwili kwa waandaaji wa
mashindano ya Iringa Super Cup yanayoshirikisha timu mbalimbali katika wilaya
ya Iringa mjini.
Akikabidhi mipira hiyo ikiwa
ni sehemu ya mchango wao kwa waandaji wa michuano hiyo, mkuu wa Takukuru mkoa wa
Iringa Emma Kuhanga amewataka vijana kuwa mstari wa mbele kupiga vita rushwa
ambayo ni adui wa haki.
Kwa upande wake mratibu wa
mashindano hayo Abu Majeki amesema mipira iliyotolewa ni ishara ya michuano
hiyo kuungwa mkono na wadau wa mchezo huo huku akiishukuru Takukuru kwa kuwajali
vijana wa makundi yote.
0 comments:
Post a Comment