Mfanyikazi wa zamani wa shirika la kijasusi la Marekani, CIA,
amejitambulisha kuwa ndiye aliyefichua taarifa kuhusu mipango ya
nchi hiyo ya kupeleleza kisiri taarifa za simu na mitandao.
Gazeti la
Uingereza la The Guardian lilifichua kuwa shirika hilo la kijasusi
limekuwa likifuatilia kisiri taarifa za watu kwa kudokoa kupitia simu na
kwenye mitandao.
Edward Snowden mwenye umri wa miaka 29
amekiri hapo jana kuwa ni yeye ndiye aliyelifichulia gazeti hilo taarifa
hizo za kijasusi katika video iliyotolewa na mtandao wa gazeti hilo.
The Guardian limesema lilitoa video hiyo kwa idhini ya Snowden
ambaye ametorokea Hong Kong.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment