Main Menu

Wednesday, June 10, 2015

TUZO ZA VODACOM PREMIER LEAGUE PASUA KICHWA



Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa kushirikiana na wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, kesho siku ya alhamis tarehe 11/06/2015 wanatarajia kutoa zawadi kwa washindi wa Vodacom Premier League msimu wa 2014/2015.

Mgeni rasmi katika halfa hiyo ya utoaji zawadi kwa wachezaji, makocha, na timu washindi atakua ni Juma Nkamia, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Vodacom watatoa zawadi kwa Bingwa wa Ligi Kuu msimu 2014/2015, mshindi wa pili, mshindi wa tatu na mshindi wa nne, baadhi ya vipengele vitakavyotolewa zawadi pia na wadhamini hao wa Ligi Kuu ni :

1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
    i.        Mohamed Hussein (Simba SC)
   ii.        Mrisho Ngasa (Young Africans)
 iii.        Saimon Msuva (Young Africans)

2. Mlinda mlango bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
    i.        Mohamed Yusuph (Tanzania Prisons)
   ii.        Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
 iii.        Shaban Hassan (Coastal union)

3. Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
    i.        Goran Kopunovic (Simba SC)
   ii.        Hans Van Der Pluijm (Young Africans)
 iii.        Mbwana Makata - (Tanzania Prisons)

4. Mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
    i.        Israel Mjuni Nkongo
   ii.        Jonesia Rukyaa
 iii.        Samwel Mpenzu

5. Timu yenye nidhamu Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
    i.        Mgambo JKT
   ii.        Mtibwa Sugar
 iii.        Simba SC

0 comments:

Post a Comment