Main Menu

Wednesday, June 10, 2015

JOHN MAHUNDI ATWAA TUZO YA PILI KWA KUWA MCHEZAJI BORA MWEZI MEI



 
Wakati huo huo mchezaji John Mahundi wa timu ya Coastal Union amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Mei, 2015 na jopo la makocha kufuatia kuwazidi wachezaji wengine 14 aliokuwa anananiwa nao nafasi hiyo.

Kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi mei, Mahundi atazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

John Mahundi hii ni mara ya pili kutwaa tuzo hiyo baada ya kufanya hivyo mwezi December.

Tuzo hizi zimekua haziendi kwa watu sahihi na kuibua maswali mengi kwa wapenzi wa soka hususani mwezi wa tatu pale alipopewa mchezaji wa Tz prison ambaye hana uhakika wa namba na muda mwingi yupo benchi hali iliyowashangaza hata wachezaji wenzake.

Nafikiri TFF inabidi iangalie utaratibu mzuroi wa kuwapata wachezaji hawa ambao mwisho wa siku ndio wanatakiwa wawe nominez wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka.

0 comments:

Post a Comment