Watanzani wametakiwa kuwapigia kura nyingi kadri wawezavyo,
wawakilishi wao katika shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’
linaloendelea nchini Afrika Kusini ili kuhakikisha wanaendelea kubaki
‘mjengoni’ wakipeperusha bendera ya taifa.
Wito huo, umetolewa na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Airtel
Tanzania, inayodhamini shindano hilo,Jackson Mmbando, huku akiwataja
wawakilishi hao wa Tanzania kuwa ni Feza Kessy na Ammy Nando.
Mmbandoalisema kuwa, ili kuendelea kumbakisha Feza katika
kinyang’anyiro cha BBA ‘The Chase,’ Watanzania wanapaswa kutuma ujumbe
wenye jina ‘FEZA’ kwenda namba 15456,
ili kumuokoa mshiriki huyo aliyeingia mara mbili kikaangoni, tofauti
na Nando(22), ambaye anafanya vizuri.
“Watanzania tuna kila sababu za kuwapigia kura wawakilishi wetu, ili
waweze kuwakilisha vema na kipaumbele zaidi kiwe kwa kumpigia Feza kwa
kuandika jina lake kwa herufi kubwa “FEZA” kisha kwenda kwa namba
15456,” alisema Mmbando.
Mshindi wa mwaka huu, atajinyakulia kitita cha Dola za 300,000 za
Marekani.Tangu shindano hilo lianze ni Mtanzania Richard, ndiye pekee
aliyewahi kushinda shindano hilo.
Mashindanohayo yanayofanyika kwa mara ya nane, yanashirikisha
washiriki 24 kutoka nchi 14za Afrika na watakaa ndani ya nyumba hiyo
kwa siku 90, ambako kusalia kwao mjengoni kunategemea kura za
watazamaji wa shindano hilo.
Katikahatua nyingine, Mmbando aliwataka Watanzania kuendelea kulipia
huduma zao zaDSTV kupitia Airtel money, kwani kuna kuna kitu cha ziada
kinakuja kwa ajili yao.
“Airtel ili kuleta burudani zaidi kwa wale wanaolipia huduma na
vifurushi vya kila mwezi vya DSTV kupitia huduma ya Airtel Money kuna
mambo mazuri yenye kuvutia yanakuja yatakayowafanya waendeleee
kutosheka zaidi kupitia huduma zetu zote” alimaliza kwa kusema bw,
Mmbando.
0 comments:
Post a Comment