Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za
kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Pan Africans, Simba na Taifa
Stars, Abdallah Msamba kilichotokea juzi usiku (Juni 12 mwaka huu)
jijini Dar es Salaam.
Msiba
huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti
Msamba akiwa mchezaji, na baadaye kocha wa timu kadhaa alitoa mchango
mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea na kufundisha ikiwemo Villa
Squad, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF
inatoa pole kwa familia ya marehemu Msamba, Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya
Kinondoni (KIFA) na klabu ya Villa Squad na kuwataka kuwa na subira na
uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Maziko
ya mchezaji huyo yamefanyika leo (Juni 14 mwaka huu) katika makaburi ya
Ndugumbi mkoani Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji
wakiwemo wachezaji wa zamani na viongozi mpira wa miguu nchini. Mungu
aiweke roho ya marehemu Msamba mahali pema peponi. Amina
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment