Askari polisi na wanajeshi wa Misri hawatashiriki kwenye uchaguzi wowote
hadi mwaka 2020.
Bunge la Misri limesitisha hadi mwaka 2020 mpango wa
kuwapa wanajeshi na askari polisi wa nchi hiyo haki ya kupiga kura.
Awali Naibu Waziri wa Ulinzi anayehusika na masuala ya sheria na katiba
wa Misri alitoa pendekezo kwa kamati ya bunge la nchi hiyo kuandaa
mpango wa kuwapatia wanajeshi na askari polisi haki ya kupiga kura
kwenye chaguzi mbalimbali zitakazofanyika nchini humo.
Mahakama ya
Katiba ya Misri mwezi Mei mwaka huu ilitangaza kuwa, kwa mujibu wa
katiba mpya ya nchi hiyo, askari polisi na wanajeshi wana haki ya
kushiriki kwenye chaguzi nchini humo.
Monday, June 10, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment