Msemaji wa Rais wa Afrika Kusini amesema kuwa, hali ya kiafya ya Nelson Mandela, Rais wa zamani wa nchi hiyo inazidi kuboreka.
Mac Maharaj amesema kuwa, ijapokuwa hali ya kiafya ya Mandela ni
mahututi, lakini sasa inatia moyo baada ya kuendelea kupata matibabu.
Maharaj amesema kuwa, Rais Jacob Zuma jana alikwenda kumjulia hali Mzee
Mandela kwenye hospitali ya Med - Clinic mjini Pretoria.
Tarehe 18 Julai siku Mandela alitimiza miaka 95 ya kuzaliwa, Rais
Zuma alilihutubia taifa na kusema kuwa, hali ya kiafya ya Mzee Mandela
inaanza kuboreka hatua kwa hatua.
Nelson Mandela ambaye anapewa heshima
kubwa na wananchi wa nchi hiyo, alikuwa rais wa kwanza mweusi baada ya
kuangushwa utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994 nchini Afrika Kusini.
Mandela aliwahi kutumikia kifungo cha miaka 27 jela tokea mwaka 1962
hadi 1990, kutokana na harakati za ukombozi dhidi ya utawala wa
kibaguzi wa wazungu wachache nchini humo.
NA radio tehranswahili
Tuesday, July 23, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment