Main Menu

Tuesday, July 23, 2013

WACHEZAJI NA WAAMUZI WALIOPANGA MATOKEO NCHINI NIGERIA WAFUNGIWA MAISHA KUJIHUSISHA NA SOKA

Shirikisho la soka nchini Nigeria limewafungia kifungo cha maisha kujihusisha na masuala ya soka wachezaji na waamuzi waliohusika kwenye mechi yenye utata iliyohusisha timu za  Plateau United Feeders, Akurba FC ,Police Machine na Bubayaro FC.
 
NFF
imesema imefanya uchunguzi wa kutosha na kupitia maelezo ya mchezo na imegundua kuwa kuna vitu visivyo vya kawaida vilifanyika na hivyo shirikisho hilo limeamua kutoa adhabu hiyo kama fundisho .

Timu zote nne zimefungiwa mechi kumi za ligi daraja la kwanza pia picha za wachezaji na waamuzi  zimetumwa kwenye shirikisho la soka barani afrika CAF na shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA ili kuwazuia wasicheze popote duniani.

mechi hizo za  mtoano za ligi daraja la kwanza kuwania kupanda ligi kuu zilitoa matokeo ya ajabu Plateau United Feeders iliifunga  Akurba FC magoli 79 kwa 0 wakati Police Machine iliifunga FC Bubayaro FC kwa magoli 67 kwa 0.

0 comments:

Post a Comment