Main Menu

Tuesday, July 23, 2013

CHAMA CHA WAFANYAKAZI WILAYA YA KILOLO CHAMJIA JUU MWANDISHI WA GAZETI LA DARAJA LETU KWA MADAI YA KUTUMIWA NA MKUU WA WILAYA HIYO.

Sakata linalomuhusu mkuu wa wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa limeeendelea kuchukua sura mpya, baada ya Chama cha wafanyakazi wilayani humo (TALGWU) kudai kuwa mkuu huyo anawatumia waandishi wa habari kupotosha ukweli wa tuhuma zinazomkabili.

Wakizungumza jana na waandishi wa habari kwenye ofisi za IPC mkoa wa Iringa, mwenyekiti wa TALGWU wilaya ya Kilolo Andrea Mwandimbile na mjumbe wa chama hicho Oscar Mwanjala wamekanusha taarifa iliyochapishwa na gazeti la Daraja letu la tarehe 22 july 2013 kwa madai kuwa hazina ukweli.

Wamesema mwandishi wa gazeti hilo ameitumia vibaya kalamu yake kwa kutumiwa na mkuu huyo wa wilaya na ndio maana ameshindwa kuhoji upande wa pili na kuandika mambo ambayo hakuyafanyia uchunguzi na kupotosha ukweli.


Aidha viongozi hao wamemtaka mkuu wa wilaya hiyo Gerald Guninita kuacha kuwatumia waandishi wa habari kupotosha ukweli wa mambo na badala yake atafute njia sahihi za kumaliza tuhuma zinazomkabili, kwani kukimbilia kwake kwenye vyombo vya habari hakutamsaidia.

Sakata hilo limeibuka mara baada ya mkuu huyo wa wilaya, kudaiwa kuwanyanyasa wafanyakazi wa halmashauri ya wilaya hiyo kwa kuwaweka ndani watumishi wawili, huku akidai kutishiwa maisha kutokana na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali.


0 comments:

Post a Comment