Mke wa mjukuu wa mfalme wa Uingereza, Prince William
amejifungua mtoto wa kiume katika hospitali ya St.Mary's, Paddington
Mashariki mwa mji wa London.
Baba wa Mtoto, Prince William alishuhudia wakati mtoto akizaliwa.
Tangazo la kuzaliwa kwa mtoto limetolewa na kuonyeshwa mbele ya lango kuu la Kasri kuu la kifalme la Uingereza la Buckingham kama utamaduni na mila za Uingereza zilivyo.
Taarifa rasmi iliyosainiwa na jopo la madaktari bingwa kuthibitisha kujifungua kwa Duchess wa Cambridge ilipelekwa kwenye kasri la kifalme chini ya ulinzi wa polisi.
Malkia wa Uingereza,Duke wa Edinburgh,Prince wa Wales, Duchess wa Cornwall na Prince Harry pamoja na wanandugu wa familia zote wametaarifiwa juu ya kujifungua salama kwa Kate na wote wamepokea vizuri habari hii, Imesema taarifa hiyo ya Kasri la kifalme.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ujumbe wa kuwapongeza Prince William na mkewe kwa kupata mtoto wa kiume na kusema nchi nzima itashangilia kwa ujio wa mtoto wa kiume.
Kiongozi wa chama cha Labour Ed Miliband pia ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter "pongezi nyingi kwa Duke na Duchess wa Cambridge.Nawatakia wao na mtoto wao furaha na afya njema."
na bbcswahili.com
0 comments:
Post a Comment