Main Menu

Saturday, October 12, 2013

SERIKALI YASAINI LESENI YA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA MADINI NCHINI LEO


Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini wakisikiliza maelezo toka kwa mmoja wa wawekezaji waliofika kuchukua leseni za utafutaji wa mafuta pamoja na uchimbaji wa madini, kushoto kwa waziri ni Kamishna wa Nishati na maendeleo ya petroli Enjinia Hosea Mbiseakifuatiwa na Kamishna wa Madini injinia Ally Samaje.
Waziri wa Nishati na Madini na Kamishna wa Nishati wakisaini leseni ya utafutaji wa mafuta mara baada ya waziri kuridhika kwa maelezo aliyoyapata toka pande zote na kuona kuna manufaa kwa nchi.
Waziri wa Nishati na Madini na Meneja wa Afrem Tanzania wakisaini leseni ya utafutaji wa mafuta kila mmoja katika kipengele chake ili kukamilisha zoezi na kuendelea na kazi kwa manufaa ya nchi wakiongozwa na wanasheria toka TPDC na Waizarani.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo leo amesaini leseni yamafuta na nyingine za madini ofisini kwake ili kuwezesha shughuli za utafutaji w mafuta na uchimbaji wa madini kuendelea na kusaidia katika kukuza uchumi wa nchi.

Leseni ya utafutaji wa mafuta iliyo chini ya Shirika la Maendeleo ya mafuta na Petroli Tanzania (TPDC) kitalu cha tanga waliokubaliana na TPDC kufanya kazi kwa pamoja (Production Sharing Agreement) na Kampuni ya Afrem Gabon katika shughuli za utafutaji wa mafuta imesaini rasmi mkataba wa kuipa kazi kampuni ndogo ijulikanayo kama Afrem Tanzania ili kuendesha shughuli zilizokuwa zikiendeshwa na shirika mama Afrem Gabon.

Aidha Profesa Muhongo amesaini leseni nyingine za madini za kampuni ya Pacco Gems Limited waliofika kuomba leseni ya uchimbaji wa madini ambapo walitakiwa kuelewa tozo mbalimbali zinazotozwa na serikali mara baada ya kuanza uzalishaji ikiwa ni pamoja na mrabaha pamoja na corporate task.

Profesa Muhongo aligoma kusaini baadhi yaleseni zilizofikishwa mezani kwake kutokana na sababu tofautitofauti ikiwemo ya waombaji wa leseni wa kampuni ya Tanga sement kutokueleza bayana kwamba katika uchimbaji wao watachimba udongo mwekundu pamoja na lime stone inayopatikana katika eneo husika na ikiwa ni rasilimali ya muhimu katika kampuni yao hivyo kutaka marekebisha ya leseni hiyo yafanyike ndipo leseni isainiwe.

Muhongo hakukubaliana na makubaliano yaliyofanywa baina ya Ahmed Mbarak mtanzania aliyefika ili kubadilisha umiliki wa leseni baada ya kumpata mshirika wa kampuni inayomilikiwa na wachina na kukubaliana kumpa asilimia 8 katika mgawo wa mapato yatokanayo na uwekezaji huo kiasi ambacho hakikumfurahisha Waziri Muhongo kutokana na utajiri uliopo katika eneo husika.

Muhongo alitaka kujua ni kwanini apewe asilimia hizo na wakati yeye ndiye mwenye eneo ndipo Qiang Gao alipozungumzia suala la Mbarak kutochangia chochote katika uwekezaji huo jibu ambalo halikumshawishi Profesa kukubaliana na hoja hiyo na hivyo kuwaataka wajadiliane upya na kurudi kusainiwa mkataba huo pindi asilimia hizo zitakapo ongezwa katika mgawo huo kinyume cha hapo mkataba huo hautasainiwa mpaka atakapopatikana mbia atakayetoa dau la juu kwa mwenye eneo husika.

Kwa upande wake Kamishna wa madini Ally Samaje alisema leseni kama hizi zinaandaliwa mara baada ya wahusika kufikia makubaliano na kufika wizarani kuomba kufanya transfer ya umiliki wa leseni husikika kwa asilimia walizokubaliana.

Profesa Muhongo amewaasa watanzania kutofanya maamuzi kutokana na shida na uhitaji walionao kwa sasa na hivyo kuwafanya wasiangalie mbele ili kuweza kupunguza migogoro mbalimbali na huko mbele kujiona kuwa hawanufaiki na rasilimali walizonazo na kumbe makosa wameyafanya wao pindi walipokuwa wakifanya maamuzi ya kuuza au kuingia ubia katika uchimbaji wa madini na rasilimali mbalimbali zilizoko nchini kwa maeneo wanayoyamiliki.


0 comments:

Post a Comment