Kocha wa klabu ya Chelsea
inayoshiriki ligi kuu ya England Jose Mourinho amekimbia kwenye kikao cha
waandishi wa habari kuelekea kwenye
mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Steaua Bucharest.
Mourinho hakufurahishwa na
maswali ya waandishi wa habari juu ya kutomjuisha kiungo wa kimataifa wa
Ubeligiji Kevin De Bruyne ambaye hajasafiri na Chelsea kwenda nchini Romanian.
Siku za hivi karibuni
Mourinho ameonekana kuchoshwa na maswali ya waandishi wa habari juu ya kwanini
hawatumii nyota kama Juan Mata na De
Bruyne.
Mourinho mwenye umri wa
miaka 50 anaingia kwenye pambano la leo akiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa
na timu ya Fc Basel ya kwenye ufunguzi wa ligi ya mabingwa barani ulaya
iliyochezwa Stanford bridge wiki 2 zilizopita.
BARCELONA NA MATUMAINI YA USHINDI LEO
Mkurugenzi wa ufundi wa
Barcelona Andoni Zubizarreta anafikiri timu yake itacheza vizuri kwenye mchezo
wa leo itakapo pambana na Celtic bila mshambulaji Lionel Messi ambaye anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja.
Zubizarreta anapata jeuri
kwa kikosi kikubwa kilichopo chini ya kocha
Gerardo Martino ambacho kinaweza kufanya kazi nzuri bila uwepo wa
mchezaji bora mara 4 wa dunia.
Zubizarreta ambaye ni
golkipa wa zamani wa Hispania anadhani
mashabiki wanaihofia Celtic kutokana na Barcelona kupoteza mechi ya ligi ya
mabingwa dhidi ya wasotland hao msimu
uliopita.
Msimu Barcelona ilifungwa
magoli 2 kwa 1 na timu ya Glascow Celtic kwenye pambano la ligi ya mabingwa lililochezwa kwenye uwanja wa Celtic Park .
NA MVP Issa maeda
0 comments:
Post a Comment