Monday, September 16, 2013
WACHEZAJI WA YANGA WATEMBELEA KIWANDA CHA BIA CHA TBL MKOANI MBEYA
Kikosi cha Yanga leo mchana kilifanya ziara kiwanda cha TBL Mbeya, kilichopo maeneo Iyunga. Katika ziara hiyo, wachezaji walipata fursa ya kujionea mambo mb alimbali, ikiwemo mfumo mzima wa utayarishwaji bia hadi kupakiwa tayari kuingia sokoni.
Walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali wakati wanatembezwa kwenye kiwanda hicho na wafanyakazi wa TBL Mbeya na kwa ujumla ilikuwa ziara yenye maufaa kwao.
Wafanyakazi wa TBL Mbeya walifurahi kukutana na wachezaji wa Yanga na wengine walichukua fursa hiyo kupiga nao picha za ukumbusho.
Kwa upande wake, Meneja Matukio wa Kampuni hiyo mjini hapa, Godfrey Mwangungula alisema kwamba kiwanda cha TBL Mbeya kinashikilia tuzo ya kiwanda bora Afrika kwa miaka mitatu mfululizo- hivyo ni faraja kwao kutembeleaa na mabingwa wa Tanzania.
Yanga kwa pamoja na wapinzani wao wa jadi, Simba SC na timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars- wote wanadhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager inayozalishwa na TBL.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment