Mshindi wa nyumba ya pili ya Airtel
Yatosha yenye thamani ya shilingi milioni 65/- amekabidhiwa cheti cha
ushindi leo ikiwa ni uthibitisho maalum mbele ya wanahabari ambapo ni
muda mfupi baada ya mshindi huyo kuibuka mshindi kupitia droo kubwa
ya mwisho wa mwezi iliyochezeshwa wiki iliyopita
Airtel Tanzania kupitia promosheni hiyo imekuwa ikitoa zawadi
mbalimbali kwa wateja wake zikiwemo pesa taslim pamoja na nyumba 3
ambapo kila mwezi nyumba moja huenda kwa mshindi mmoja .
Akizungumza kwa furaha Mshindi wa nyumba hiyo ya pili Bi Anna Gustav
Lyimo ambae ni mkazi wa Dar es salaam alisema “namshukuru sana Mungu
kwa kuniwezesha kuwa mshindi wa nyumba ya Airtel Yatosha,
Nilipopigiwa nilijua ni matapeli, mpaka siku ya pili nilipopigiwa kwa
mara ya pili na Airtel ndipo nilipojua si utapeli”
“Nawashukuru sana Airtel kwa zawadi hii kwani imenirahisishia mipango
yangu ya kuanza ujenzi wa Nyumba mwishoni mwa mwaka huu. ,”
alisisitiza Bi, Lyimo
“Ninawashauri wateja wengine wa airtel kuendela kutumia huduma ya
Airtel yatosha ili na wao waibuke washindi kama mimi” alimalizia
kusema Bi Anna Lymo
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema
“makabidhiano ya cheti hiki ni taratibu za awali ambapo hivi karibuni
mshindi huyu atakabidhiwa rasmi nyumba yake iliyopo maeneo ya
Kigamboni jijini Dar es salaam.
“Airtel tutaendelea kutoa zawadi bora kwa wateja wetu nchi nzima
kupitia promosheni mbalimbali tulizonato”
“Kama alivyo na furaha mshindi wetu ndivyo na sisi tunavyofurahi na
hii sio kikomo bado tunatoa zawadi za pesa taslim kila siku kwa wateja
mbalimbali wa Airtel nchi nzima. Njia ni rahisi tu! Jiunge sasa na
vifurushi mbalimbali vinavyopatikana kupitia Yatosha na utapata nafasi
ya kuingia kwenye droo ya kushinda,” alisema Mmbando.
Kujiunga na vifurushi hivyo mteja anapaswa kupiga *149*99# na kuchagua
1 au 2 kisha aweze kujiunga na kifurushi chochote cha Wiki, Siku au
Mwenzi.
Airtel kupitia promosheni ya Airtel yatosha imeshatoa zaidi ya
shilingi milioni 60 kwa wateja wake kupitia promosheni hii ambapo
Promosheni hii inadumu kwa siku 90 toka ianze, hadi sasa bado kuna
nyumba moja kati ya tatu zilizopo Kigamboni itashindaniwa kwa mwezi
huu.
Wanahabari wakirekodi tukio wakati Anna G. Lyimo anakabidhiwa cheti chake cha nyumba leo jijini Dar es salaam.
Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmmbando (kushoto) akiongea na wanahabari kabla ya kukabidhi cheti Mshindi wa Nyumba ya pili ya Airtel Yatosha Anna G. Lyimo (kati)
Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmmbando (kushoto) akimkabidhi cheti Mshindi wa Nyumba wa Airtel Yatosha bi. Anna G.Lyimo mkazi (kulia) wa Dar Es Salaam akishuhudiwa na Meneja masoko wa Airtel Tanzania Anethy Muga.
Mshindi wa Nyumba wa pili wa Airtel Yatosha bi. Anna G. Lyimo akionyesha cheti chake alichokabidhiwa na Meneja wa uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (kulia), wakishuhudiwa na Meneja masoko wa Airtel Anethy Muga (kushoto)
0 comments:
Post a Comment