Main Menu

Friday, September 13, 2013

SEMINA YA KAMATA FURSA TWENDE ZETU KWA VIJANA YAFANYIKA LEO MKOANI DODOMA.


Msanii mahiri wa Kughani Mashairi kwa mtindo wa kisasa kabisa,Mrisho mpoto akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake waliojitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya kamata Fursa twendzetu,iliofanyika ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma. Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group,imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo  Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara,Mbeya,Iringa sambamba na leo ndani ya Dodoma,ambo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.
 Sehemu ya washiriki wa semina hiyo ilipokuwa ikiendelea mapema leo asubuhi.


 Mwakilishi wa NSSF-Makao Makuu,Salim Khalfan akifafanua masuala mbalimbali yatokanayo na faida za kujiunga na shirika hilo la NSS,ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu iliofanyika mapema leo kwenye moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
  Sehemu ya ya watu wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo.
 Meneja wa  NSSF mkoani Dodoma,Bwa.Kirondera Nyabuyenze akizungumza fursa mbalimbali zitokanazo na shirika la NSSF,Nyabuyenze amewataka watu mbalimbali wajitokeze kwa wingi kujiunga na NSSF,ili kujipatia fursa mbalimbali zikiwemo mikopo,matibabu na mambo mengiyo mbalimbali.
 Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Maxmalipo,Bernard Munubi akizungumza kwenye semina ya Kamata Fursa Twenzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala mbalimbali yanayofanywa na kampuni yake katika kusaidia huduma za jamii,ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.


0 comments:

Post a Comment