Chama
cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kimemjia juu balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing kutokana na ushiriki wake katika mkutano wa hadhara wa chama cha mapinduzi CCM uliofanyika hivi karibuni wilaya ya Kishapu.
Chama hicho kimewaeleza wandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa kitendo cha balozi huyo kushiriki katika mkutano huo huku amevaa kofia yenye nembo ya chama tawala ni kinyume cha mkataba wa kimataifa wa Viena Convention ambao unakataza mabalozi kujihusisha na masuala ya nchi husika.
Kufuatia hali hiyo Mkurugenzi wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa chadema Ezekiel Wenje amesema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ili iwe fundisho kwa chama cha mapinduzi na mabalozi wengine wenye tabia kama hiyo.
Akitilia mkazo hatua hiyo Mkurugenzi wa masuala ya bunge na halimashauri wa chadema John Mrema ameonyeshwa kushangazwa na kitendo hicho ambacho ni hatari kwa ushirikiano wa kati ya Tanzania na China.
Balozi Youqing anadaiwa kushiriki katika mkutano wa chama cha mapinduzi uliofanyika Septemba 13 wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanya, kwa kutoa hotuba na kushiriki shughuli za chama hicho ikiwa pamoja na kucheza rhumba sambamba na baadhi ya viongozi wa chama tawala wakiongozwa na katibu Mkuu Abdurahman Kinana
Monday, September 16, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment