Shirika la upelelezi la Marekani, FBI, limemtambua
mwanaume aliyewauwa watu 12 kwenye kituo cha jeshi la
majini mjini Washington jana.
Mtu huyo, Aaaron Alexis,
mwenye umri wa miaka 34, aliwauwa watu hao kwa
kuwapiga risasi, na yeye mwenyewe akauawa katika kisa
hicho. FBI imesema inaamini mtu huyo aliwahi kuwa askari.
Awali polisi ilikuwa ikiwasaka watu wawili kwa tuhuma za
mauaji hayo, lakini baadaye iling'amua kuwa mmoja wao
hakuhusika. Mkuu wa polisi mjini Washington, Cathy Lanier,
amesema bado hawajui sababu iliyosababisha mauaji hayo.
Hata hivyo meya wa Washington, Vincent Gray, amesema
hakuna sababu yoyote ya kuyahusisha mauaji hayo na
ugaidi. Katika Ikulu ya Marekani, Rais Barack Obama
amesema anaomboleza mauaji mengine ya kiholela ya
kutumia bunduki.
NA dwswahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment