Main Menu

Tuesday, September 17, 2013

BAADA YA KUIZAWADIA LIVERPOOL SARE JONJO SHELVEY AWAOMBA RADHI MASHABIKI WA SWANSEA

Kiungo wa klabu ya Swansea City inayoshiriki ligi kuu ya England Jonjo Shelvey amewaomba radhi mashabiki wa timu yake  kufuatia sare ya magoli 2 kwa 2 waliyoipata usiku wa jana dhidi ya Liverpool.

Uamuzi wa Jonjo kuomba radhi unatokana na pasi mbovu aliyoitoa  kwenda kwa mchezaji wa timu yake kumfikia nyota wa Liverpool Victor Moses ambae aliipatia goli la pili timu hiyo  aliyowahi kuichezea kabla ya kuihama msimu uliopita wa usajili.

Jonjo ambae aliifungia Swansea goli 1 na kusaidia upatikanaji wa goli lingine lililofungwa na Miguel  Perez maarufu kama  Michu amesema anaomba mashabiki wa timu yake wamsamehe kwa makosa mawili aliyoyafanya na kuifanya Liverpool kupata magoli yao mawili.

Swansea City
ndio waliokuwa wakwanza kupata goli lililofungwa dakika ya pili na Jonjo Shelvey kabla ya Liverpool kusawazisha kuitia kwa Danniel Sturrige  dakika ya 4 huku Victor Moses kuifungia Liverpool goli la pili dakika ya 34 lakini Michu akaisawazishia Swansea City dakika ya
64.

0 comments:

Post a Comment