Main Menu

Tuesday, September 17, 2013

CHAMA TAWALA NCHINI RWANDA CHAONGOZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA BUNGE ULIOFANYIKA JANA

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa Bunge uliofanyika jana nchini Rwanda yanaonesha kuwa chama tawala cha RPF-Inkotanyi kinaelekea kupata ushindi mkubwa.

Matokeo ya awali yaliyotolewa usiku wa kuamkia leo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi yanaonesha kuwa chama cha RPF na washirika wake wamepata asilimia 76.07 ya asilimia 75 ya kura zote zilizopigwa hadi kufikia usiku wa kuamkia leo.

Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Rwanda Prof. Kalisa Mbanda amesema kuwa matokeo kamili ya awali ya uchaguzi wa jana wa Bunge yatatolewa leo mchana.

Chama cha Social Democratic Party (PSD) ni cha pili kwa kupata asilimia 13.01 ya kura kikifuatiwa na Liberal Party (PL) ambacho kimepata asilimia 9.38.

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa Bunge wa Rwanda yatatangazwa Septemba 25. 

NA radio tehranswahili

0 comments:

Post a Comment