Aliyepata
kuwa Mkurugenzi wa Fedha TFF na Mtaalamu wa masuala ya fedha, hisa na kodi
Bwana Silas Mwakibinga amesema kuwa mfumo wa Majimaji Kampuni na kuingizwa
kwenye soko la hisa kutakuwa mfano kwa klabu za Tanzania kuona jinsi ambavyo
ubabaishaji unaweza kumalizwa kwenye soka.
Bwana
Mwakibinga amesisitiza kuwa ili ubabaishaji uishe katika mpira wa Tanzania ni
lazima iwepo klabu ya mfano na Majimaji FC inachokifanya kuingia kwenye Kampuni
na hisa zake kuuzwa ndio kile ambacho Watanzania wanakitaka.
“Unajua
vilabu vyetu vimekuwa na ubabaishaji kutokana na kukosa mfumo unaoeleweka. Lakini
Majimaji FC Kampuni na kuingia kwenye soko la hisa kutalazimisha kutoa mapato
na matumizi kwa mujibu wa sheria ya soko la hisa kila mwezi jambo ambalo tayari
linaondoa ubabaishaji wowote ule.” Alisema Mwakibinga.
Aidha
Mwakibinga amewataka wafadhili mbalimbali ambao wanataka kuwekeza kwenye soka
kujiandaa kuweka fedha zao Majimaji kwakuwa watapata taarifa zote za uendeshaji
wa klabu kwa mujibu wa sheria.
“Sheria
itailazimisha Majimaji kutoa mapato na matumizi lakini vilabu vingine vinaingia
kwenye migogoro kwa sababu hakuna utaratibu huo kwao na hawalazimishwi na
sheria.”
Tayari
wadau mbalimbali wamekwishathibitisha kushiriki katika Majimaji Revival
Conference, mkutano wa kujadili mfumo na mikakati ya kiuendeshaji ambayo
itajengwa kwaajili ya Majimaji FC Kampuni itakayozaliwa tarehe 10 Agosti 2013
katika ukumbi wa Centenary chini ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Mwambungu.
Pamoja
na Silas Mwakibinga mtoa mada mwingine katika Majimaji Revival Conference
anatarajiwa kuwa Dkt Damas Ndumbaro, Mwanasheria na wakala wa kimataifa wa
FIFA.
Imetolwa
na;
Tanzania
Mwandi Co Ltd.
Phone:
+25522 2120677 or +255756 829071
Fax:
+255 22 2122976
Email:
ceo@tanzaniamwandi.co.tz,
Website: www.tanzaniamwandi.co.tz/events.html
0 comments:
Post a Comment