Katibu wa Itikadi na Uenezi (Nec-CCM), Nape Nnauye, ametuhumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa haitendi haki kwa kuwazuia wajumbe wa Baraza la Katiba kusoma waraka wa chama hicho unaopinga baadhi ya mambo yaliyopo kwenye rasimu.
Nape alitoa shutuma hizo jana alipozungumza kwa
njia ya simu, alibainisha kuwa viongozi wa Jukwaa la Katiba akiwamo
Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba, wanataka mapendekezo yaliyopo
kwenye rasimu yapite yalivyo.
“Kwani kufanya hivyo wanazuia maoni ya wananchi,
ingawa hatujawatuma kuusoma kwenye mapendekezo, lakini wana haki ya
kuutumia wanavyojisikia,” alisema Nape.
Alisema wanajua wapo watu wachache wanaoupinga waraka huo wa CCM, lakini hawaelewi kwa sababu unahusu wanachama wao.
“Tume itende haki isikilize mawazo ya kila mtu,
inachofanya sasa ni ubaguzi, wao wanatakiwa kusikiliza maoni siyo
kutetea rasimu,” alisema.
Hivi karibuni vyombo vya habari viliripoti jinsi
Jaji Warioba alivyokosoa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba wanaokwenda na
matamko au nyaraka za vyama, badala ya maoni ya wananchi waliowachagua.
NA gazeti mwananchi
NA gazeti mwananchi
0 comments:
Post a Comment