Leo Japan inafanya kumbukumbu ya miaka 68 tangu kutokea shambulizi la
bomu la Nuklia katika eneo la Hiroshima.
Kiasi watu 50,000 waliohudhuria
kumbukumbu hiyo walikaa kimya kwa dakika moja kutowa heshima kwa
maelfu ya watu waliouwawa katika tukio hilo la kihistoria lililoshuhudiwa mwaka
1945 siku kama ya leo.
Mashambulio mengine ya silaha ya bomu la Nuklia
yalishuhudiwa siku tatu baadae katika eneo la Nagasaki nchini humo katika
mwaka huohuo ambapo maelfu ya wajapan zaidi waliuwawa hatua
iliyoichochea nchi hiyo kusalimu amri katika vita vya pili vya dunia.
Waziri mkuu
Shinzo Abe akiwa ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria kumbukumbu
hizo amesema nchi yake kama mhanga pekee wa shambulio la bomu la
Nuklia,ina jukumu la kutafuta njia za kumaliza uwepo wa silaha hizo.
NA dwswahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment