Maafisa nchini Uhispania wamemkamata mwanamume
anayetuhumiwa kuwanajisi watoto 11 walio kati ya umri wa
miaka 4 na 15 nchini Morocco aliyeachiliwa hivi karibu
baada ya kusamehewa na mfalme wa Morocco.
Daniel
Galvan Vina anatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama
kuu nchini Uhispania hii leo.
Vina alikuwa akitumikia kifungo
cha miaka 30 kabla ya mfalme Mohammed wa sita
kumsamehe pamoja na wafungwa wengine 48 raia wa
Uhispania wiki iliyopita.
Taarifa za kuachiliwa kwake zilizua
maandamano makubwa yaliyoambatana na ghasia nchini
Morocco na kumlazimu mfalme huyo kubatilisha uamuzi
wake.
Inasemekana mfalme Mohammed hakufahamu
ukubwa wa kosa alilofanya raia huyo mhispania wakati
akitoa amri hiyo ya kumsamehe yeye pamoja na wenzake.
na dwswahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment