Hatua
ya kwanza ya usajili wa wachezaji kwa msimu wa 2013/2014 imefungwa
rasmi jana (Agosti 5 mwaka huu) ambapo klabu zote za Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) zimewasilisha usajili wa vikosi vyao ndani ya wakati.
Baadhi
ya klabu zimefanya makosa madogo madogo katika usajili ambapo zimepewa
siku ya leo (Agosti 6 mwaka huu) kufanyia marekebisho kasoro hizo. Hivyo
kesho (Agosti 7 mwaka huu) majina ya vikosi vyote yatabandikwa kwenye
mbao za matangazo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa
ajili ya kipindi cha pingamizi kitakachomalizika Agosti 12 mwaka huu.
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa
itakutana Agosti 13 na 14 mwaka huu kupitia na kufanyia uamuzi usajili
wa wachezaji wenye matatizo.
Hatua
ya pili ya usajili itaanza tena Agosti 14 mwaka huu ikihusisha
wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu
huu na wale kutoka nje ya Tanzania. Hivyo, dirisha la uhamisho kwa
wachezaji wa kimataifa litafungwa baada ya hatua ya pili ya usajili
kumalizika Agosti 29 mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment